Higher Education Students' Loans Board
Zikiwa zimebaki siku kumi (10) kabla ya kufunga dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka 2025/2026, tunawakumbusha waombaji wa mikopo na ‘Samia Scholarship’ kwamba dirisha litafungwa tarehe 31 Agosti, 2025 na hakutakuwa na muda wa nyongeza.
Itakumbukwa kuwa katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika tarehe 11 Agosti 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, alisisitiza kuwa dirisha la uombaji wa mikopo lililofunguliwa tarehe 15 Juni, 2025 litafungwa rasmi tarehe 31 Agosti, 2025.
Wanafunzi, walezi, wazazi na wadau wote kwa ujumla, wanakumbushwa kuwa zimebaki siku 10 pekee kabla ya dirisha kufungwa. Hivyo, wanafunzi wahitaji wenye sifa ambao bado hawajakamilisha maombi yao wanahimizwa kufanya hivyo ndani ya muda uliobaki ili kuepuka msongamano wa dakika za mwisho.
Kwa msaada au taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya HESLB: www.heslb.go.tz, piga simu 0736 66 55 33, tuma ujumbe wa WhatsApp kupitia 0739 66 55 33 au tuma barua pepe kwenda info@heslb.go.tz
Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
Alhamisi, 21 Agosti 2025,
Dar es Salaam