Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


28
May 2025

RAIS SAMIA AONGEZA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOKA BIL 464 HADI BIL 787

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka kiasi cha shilingi bilioni 464 katika bajeti ya mwaka 2024/2025 hadi kufikia TZS 787 Bilioni katika bajeti ya mwaka 2025/2026.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma (Jumanne, Mei 27, 2025) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya serikali katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) huku akisisitiza kuwa wizara yake imeongeza vituo vingine viwili vya umahiri katika elimu tiba Afrika Mashariki vinavyotarajiwa kujengwa nchini na hivyo itawezesha vituo hivyo kuwa vitatu.

Amesema kuwa vituo hivyo kimoja kitakuwa katika Hospitqli Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kingine kitakuwa Hospitali ya Mloganzila, na hivyo kufanya kuwa na vituo vitatu vya  umahiri katika elimu tiba Afrika Mashariki.

Aidha, Waziri Mkenda amesema kuwa kinajengwa kituo cha umahiri cha elimu tiba, Sayansi ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ambapo kwa sasa Dola za Marekani Milioni 83 zimeongezwa na ujenzi utafanyika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambacho kitakuwa kituo bora kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.