Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


13
August 2024

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI: UANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA SI SIFA YA KUPATA MKOPO

Jumanne, Agosti 13, 2024

Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii, likiwemo jukwaa la ‘JamiiForums’ kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoomba mkopo wanapaswa kuwa na kadi za chama cha siasa ili kupata mkopo.

Upangaji mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) unaongozwa na Sheria ya HESLB (SURA 178) na miongozo ambayo hutolewa kila mwaka kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili na kupatikana katika www.heslb.go.tz

Sifa zinazotajwa na Sheria na miongozo ni mwombaji Awe Mtanzania; Awe ameomba mkopo; Awe amepata udahili katika taasisi inayotambuliwa na mamlaka za Serikali; Asiwe na chanzo kingine cha fedha cha kugharamia masomo; na kwa anayeendelea na masomo, awe amefaulu mitihani ya mwaka uliotangulia.

Aidha, miongozo inatoa kipaumbele kwa wahitaji kutoka katika makundi maalum kama yatima, wenye ulemavu na waliofadhiliwa katika masomo yao ya sekondari au stashahada ambao hupaswa kuthibitisha uhitaji wao kwa kujaza fomu maalum wakati wa uombaji.

Hivyo, miongozo ya mwaka wa masomo 2024/2025, kama ambavyo imekuwa katika miongozo ya miaka iliyopita, haitaji sifa ya uanachama kwa chama cha siasa kama kigezo cha kupata mkopo wa elimu ya juu.

Kwa msingi huo, tunawashauri wanafunzi wote wanaoomba mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB KUSOMA na KUZINGATIA miongozo ambayo ilizinduliwa na Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda (MB), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, siku ya Jumatatu, Mei 27, 2024 jijini Tanga na ambayo inapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz).

Imetolewa na:

Dkt. Bill Kiwia,

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Jengo la PSSSF, Barabara ya Makole,

S.L.P. 984,

DODOMA