Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


18
May 2024

UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA FEDHA ZA KUJIKIMU KWA ROBO YA NNE

Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na umma kuwa tunakamilisha malipo ya fedha za kujikimu (Chakula na Malazi) kwa robo ya nne (Quarter IV) na wanafunzi watarajie kupokea fedha hizo kuanzia Jumatatu, Mei 20, 2024.

Ufafanuzi huu unafuatia maoni na maswali yanayoulizwa na wanafunzi wanufaika kupitia barua pepe, mitandao ya kijamii kuhusu hatua ya malipo iliyofikiwa hususan kwa vyuo ambavyo tarehe za malipo (due dates) ya robo ya nne zimefika.

Aidha, tunapenda kuwasihi wanafunzi kuendelea kuwa watulivu na kuwasiliana na Maafisa Mikopo waliopo katika vyuo vyote nchini pale watakapokuwa na maoni au kuhitaji ufafanuzi.

Katika mwaka wa masomo 2023/2024, Serikali imetenga TZS 786 bilioni kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa wanafunzi zaidi ya 220,000 wanaosoma shahada na stashahada mbalimbali katika taasisi za elimu nchini.

Taarifa hii pia inapatikana katika mitandao ya kijamii ya X (zamani Twitter), Facebook na Instagram kwa jina la HESLB Tanzania.

 

Imetolewa na:

Dkt. Bill Kiwia

Mkurugenzi Mtendaji

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Jengo la PSSSF, Barabara ya Makole,

S.L.P. 984,

DODOMA

Ijumaa, Mei 17, 2024

 

#WeweNdoFuture

#TimizaWajibu