Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


1
July 2021

UFAFANUZI TAARIFA YA DENI KATIKA ‘SALARY SLIPS’

Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu wanaoendelea kurejesha mikopo kuwa makato yao katika mishahara ya mwezi Juni, 2021 yamefikishwa HESLB na kuhuishwa katika akaunti zao zilizopo HESLB.

Taarifa hii inafuatia maoni na malalamiko kutoka wa wateja wetu kuwa hawaoni kupungua kwa madeni katika hati za mishahara za mwezi Juni, 2021.

Tumewasiliana na wadau wetu, wakiwemo waajiri katika sekta ya umma, ili kurekebisha taarifa zilizoingizwa katika hati za mshahara za mwezi Juni, 2021.

Tunawashauri wateja wetu wanaorejesha mikopo kupitia mishahara, kutembelea www.heslb.go.tz katika eneo la ‘Mnufaika’ ili kupata taarifa sahihi za madeni yao na utaratibu wa malipo.

Mwisho.

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

DAR ES SALAAM

Alhamisi, Julai 1, 2021