Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


3
May 2021

Utekelezaji wa Kufutwa Tozo ya VRF

Kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kufutwa kwa Tozo ya Kutunza Thamani ya Fedha (VRF) Mei 1, 2021, tunapenda kuwataarifu wateja wetu yafuatayo:

1) Tumeanza kufanyia kazi maelekezo hayo kwa kupitia mifumo ya TEHAMA (configuration exercise) yenye taarifa za madeni ya wateja;

2) Kwa sasa, wateja wetu wawe watulivu na taarifa za ziada zitakuwa zinatolewa mara kwa mara kupitia tovuti hii na mitandao yetu ya kijamii; na

3) Kwa maswali, tuma barua pepe kwenda repayment@heslb.go.tz au WhatsApp kwa namba 0739 66 55 33

Aidha, tunapenda kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kutambua kazi tunayoifanya hususan ukusanyaji wa mikopo ambao umeongezeka kutoka TZS 28.2 bilioni (2015/2016)  hadi TZS 192 bilioni mwaka 2019/2020.

Tunaahidi kuendeleza kazi kwa kutambua kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais - KAZI IENDELEE!

 

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Dar es salaam.

Jumapili, Mei 2, 2021.