Higher Education Students' Loans Board
Tunawajulisha wanafunzi wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali hapa nchini ambao ratiba za malipo (due dates) ya mikopo yao zimefika, kuwa malipo ya fedha za mikopo yao ya chakula na malazi kwa robo ya pili ya 2024/2025 iko katika mchakato wa malipo na yanatarajiwa kukamilika ndani ya siku chache zijazo.
Aidha, kupitia taarifa hii, tunawataarifu wanafunzi ambao ratiba za malipo yao hazijafika au zinakaribia kwamba malipo yao yako katika maandalizi na yatalipwa muda utakapofika.
Utaratibu wa malipo ya mikopo ya wanafunzi kwa ajili ya fedha za kujikimu hufanyika kila baada ya siku sitini (60) hadi sabini na sita (76) ambapo wanafunzi wanufaika wanakuwa masomoni chuoni.
Hitimisho
Bodi inaendelea kuwakumbusha wanafunzi wanufaika na umma kwa ujumla kwamba mara zote inazingatia maslahi na hali bora ya wanafunzi wanaogharimiwa masomo yao kupitia mikopo ya wanafunzi kwa kuzingatia miongozo na taratibu za malipo ya fedha za umma.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Jumanne, Disemba 31, 2024
Taarifa hii pia inapatikana kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii (Facebook, Instagram na X) kwa jina la HESLB Tanzania.