Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


26
September 2024

TAARIFA KWA UMMA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  (HESLB) inawatangazia wanafunzi na watanzania wote kuwa taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii na makundi ya ‘WhatsApp’ kuhusu sifa, maeneo ya ufadhili na tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ya SAMIA SCHOLARSHIP  kwa mwaka 2024/2025 siyo sahihi na inapaswa kupuuzwa.

HESLB inaendelea kuwasisitiza wanafunzi walengwa na watanzania kwa ujumla kuwa mwongozo na taarifa sahihi kuhusu ‘SAMIA SCHOLARSHIP’ kwa mwaka 2024/2025 zinapatikana kupitia tovuti yake www.heslb.go.tz na kurasa za mitandao ya kijamii kwa jina la HESLB Tanzania.

Aidha, itakumbukwa kuwa dirisha la maombi ya ‘SAMIA SCHOLARSHIP’ kwa mwaka 2024/2025 lilifunguliwa Agosti 8, 2024 na kufungwa Septemba 14, 2024.

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano

Jumatano, Septemba 25, 2024