Higher Education Students' Loans Board
1. UTANGULIZI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kushirikiana na taasisi ya Adanian Labs inapenda kuwafahamisha wanafunzi na wahitimu wa shahada kuhusu uwepo wa fursa za mafunzo ya TEHAMA ili kuwaongezea ujuzi na kupanua wigo wa kuajirika.
Mpango huu ni sehemu ya jitihada za HESLB za kuwajengea uwezo wa kuajirika wahitimu wa shahada mbalimbali ambao pia ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa na hivyo kuwa na uwezo wa kurejesha.
2. WALENGWA
Walengwa ni wahitimu wa shahada zenye mchepuo wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na sayansi ya kompyuta (ICT and computer-related degree graduates). Aidha, wanafunzi wa kozi hizi waliopo katika mwaka wa mwisho wa masomo nao wanaweza kuomba.
3. UTARATIBU WA KUOMBA
Ili kufikiriwa kupata fursa hizo, mwombaji atapaswa kufuata njia zifuatazo:
i. Kuingia katika https://dlt.adanianlabs.io na kujisajili;
ii. Katika kujisajili, mwombaji atajaza majina yake kamili, tarehe ya kuzaliwa, namba ya mtihani wa kidato cha nne (Mfano: S.0001.0001.2024) na kufuata maelekezo mengine.
4. UTARATIBU WA KUENDESHA MAFUNZO
Kwa wanafunzi watakaochaguliwa, mafunzo yataendeshwa BURE kwa miezi minne kwa njia ya mtandao kuanzia Agosti 5, 2024. Aidha, kila mwanafunzi atapaswa kuwa na kompyuta na intaneti ili kushiriki mafunzo hayo.
5. KUTANGAZWA KWA WALIOFANIKIWA KUCHAGULIWA
Baada ya kukamilisha kuwasilisha maombi kwa mtandao, mwombaji anashauriwa kutembelea akaunti yake aliyotumia kuomba ili kufahamu hali (status) ya ombi lake. Aidha, kwa wanufaika wa mikopo ya HESLB ambao wataomba, majina yao yatatangazwa kupitia tovuti hii.
Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
S.L.P. 954, Dodoma
Jumanne, Julai 23, 2024