The United Republic of Tanzania
HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOANS BOARD

WITO WA KUWASILISHA TAARIFA ZA WANUFAIKA WALIOFARIKI DUNIA


Tunawatangazia wazazi, walezi, ndugu na wadhamini wa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu waliofariki dunia wakiwa masomoni au baada ya kuhitimu masomo, kuwasilisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) nyaraka zinazothibitisha vifo ili taratibu za kufuta baki ya madeni zikamilishwe kama sheria ya Bodi ya Mikopo (SURA 178) inaipa HESLB mamlaka ya kufuta mkopo wa mnufaika aliyefariki dunia

Nyaraka hizo ni yoyote kati ya zifuatazo iliyothibitishwa na Kamishna wa Kiapo au Mamlaka inayoitoa:

  1. Nakala ya Cheti cha Kifo (Death certificate)
  2. Nakala ya Kibali cha Mazishi (Burial permit)
  3. Barua kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji inayothibitisha kutokea kwa kifo hicho
  4. Barua kutoka Chuo alichosoma au Mwajiri wake
  5. Nakala ya Tangazo la kifo lililotolewa kwa umma (Public Notice) kupitia gazetini.

Nyaraka hizi zinaweza kuwasilishwa HESLB pamoja na barua kupitia anuani ifuatayo:


Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

S.L.P. 76068,

DAR ES SALAAM.

Barua pepe: repayment@heslb.go.tz


Aidha, tunawataarifu wazazi, walezi, ndugu na wadhamini kuwa HESLB imepokea baadhi ya majina ya wanufaika waliofariki dunia kutoka vyuoni ambayo inapatikana hapa. Wazazi, walezi, ndugu na wadhamini wao wanashauriwa pia kuwasilisha nyaraka kama ilivyoelekezwa.

 

Imetolewa na

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Januari 2, 2020,

DAR ES SALAAM.