The United Republic of Tanzania
HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOANS BOARD

ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020


HESLB imetoa orodha ya waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zina upungufu ili wafanye marekebisho kwa siku nne kuanzia kesho Jumatatu tarehe 30 Septemba 2019 ambapo pia mwongozo wa jinsi ya kufanya marekebisho utatolewa..

Hatua ya HESLB inafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo imebainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.
 

  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada ya kwanza *bofya hapa.*
  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) *bofya hapa.*
  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada za Uzamili na Uzamivu*bofya hapa.*Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
29 Septemba 2019