Home Loans Guidelines WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WATEMBELEA HESLB
WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WATEMBELEA HESLB

Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, wametembelea ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Ziara hiyo ya wawakilishi ilifanyika Machi 7, 2012 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti walikutana na wawakilishi na kuwasilisha taarifa ya utendaji wa Bodi, changamoto wanazokabiliana nazo na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo .

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wanaojiunga na taasisi za elimu ya juu zinazotambulika Tanzania Bara na Zanzibar. Tayari HESLB imefungua ofisi ya Kanda Zanzibar kwa ajili ya kuwahudumia Wanafunzi na taasisi za elimu ya juu zilizoko visiwani humo.

 
Higher Education Students' Loans Board