Tupo kwenye Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa

HESLB tupo kwenye Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam katika Banda la Katavi namba 26 na 27 tukitoa elimu kwa umma kuhusu utoaji na urejeshwaji mikopo.

Katika kipindi hicho watumishi wa HESLB walioko kwenye maonesho hayo watakuwa wanatoa huduma moja kwa moja kwa wateja ikiwa ni pamoja na kutoa ankara za madeni ya wanufaika wa mikopo.

Huduma zingine zitakuwa ni kuwaelekeza waombaji mikopo wa mwaka wa masomo 2018/2019 taratibu za ujazaji wa fomu za maombi ya mikopo na maswali mengine yanayohusu huduma za jumla za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) vilivyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam yanahusisha mamia ya taasisi za serikali na binafsi za ndani na nje ya nchi. Yamefunguliwa Juni 28 na yataendelea hadi Julai 13, 2018.

Wadau wote wa elimu ya juu mnakaribishwa kwenye Banda la Katavi namba 26 na 27.