HESLB TUPO MAONESHO YA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawakaribisha wadau wake wote kupata huduma mbalimbali katika maeneo ya Utoaji mikopo na Urejeshaji mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia tarehe 26 Julai hadi tarehe 29 Julai, 2017 kwenye Maonesho ya 12 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi chote cha maonesho hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU); Bodi ya Mikopo itatoa huduma kwa wateja katika banda lake kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni. Hii ni moja ya fursa muhimu ambapo wadau watakaofika banda la Maonesho la Bodi watajibiwa maswali na kupewa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Utoaji Mikopo hususan kwa Mwaka wa masomo 2016/2017 na maandalizi ya mwaka mpya wa masomo 2017/2018.

  • EXHIBITION
    Kuhusu Urejeshaji wa Mikopo; Taarifa za kiasi cha mkopo anaodaiwa mnufaika zitatolewa ambapo Wanufaika ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao wataweza kujaza fomu za maulizo (inquiry forms) kwa kutoa taarifa zao za sasa ili Bodi iweze kuanza kukusanya mikopo kutoka kwao.

    Kwa upande wa Utoaji mikopo; wadau watapata fursa ya kujua vigezo vinavyotumiwa, utaratibu wa kuomba hadi kupangiwa mikopo, viwango vya mikopo vinavyopangwa; utaratibu wa kukata rufaa na iwapo kuna tatizo la utoaji mikopo kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taarifa za mwombaji mkopo.

    Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu pia imeandaa machapisho yenye taarifa za utoaji na urejeshwaji mikopo ili kuwagawia wadau watakaotembelea banda lake.
     

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tarehe 25 Julai, 2017