Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


20
December 2024

HESLB MARATHON YAZINDULIWA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 20

- Kufanyika Dar Feb 15, 2025

- ⁠Rais SMZ kuongoza

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia leo  (Ijumaa, Disemba 20, 2024) amezindua mbio za hisani  kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa HESLB zitakazofanyika  Februari 15, 2025 katika Viwanja vya Farasi (Green Grounds) jijini  Dar es salaam.

Mgeni rasmi wa mbio hizo zinazojulikana kama HESLB Marathon, atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Dkt. Kiwia amesema fedha zitakazokusanywa kupitia HESLB Marathon zitatumika kununulia vifaa vya maabara ya shule mbili za sekondari; moja ya Zanzibar na nyingine ya Tanzania Bara.  Ameongeza pia kuwa kiasi kingine cha fedha kitatumika kuboresha kituo cha HESLB cha huduma za simu kwa wateja (HESLB Customer Call Centre).