Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


10
February 2023

Waziri Mhagama: Wanufaika rejesheni mikopo ya elimu ya juu

Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wametakiwa kujitokeza na kurejesha mikopo ili iwanufaishe watanzania wahitaji wengine.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema uamuzi wa mwaka 2021 wa Serikali wa kufuta tozo ya kulinda thamani katika mikopo ya elimu ya juu ulilenga kurahisisha urejeshaji.

“Baada ya Serikali kuondoa tozo ya kulinda thamani, imewarahisishia wanufaika na hivyo sasa wajitokeze na kurejesha mikopo,” amesema Waziri Mhagama wakati akikagua mabanda ya washiriki wa Kikao Kazi cha Tatu cha Mwaka kuhusu Serikali Mtandao kinachofanyika jijini Arusha.

Wakati huohuo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru amesema HESLB imepiga hatua kubwa katika matumizi ya TEHAMA katika kipindi cha miaka 17 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005.

Badru amesema hayo alipokua akiwasilisha mada katika Kikao Kazi cha Tatu cha Mwaka kuhusu Serikali Mtandao kilichofanyika jijini Arusha kuanzia Februari 8 – 10 mwaka huu.

“Mwaka 2005 hadi 2010, tulikua tunachapisha fomu na kusambaza ili waombaji mkopo wajaze na kurejesha na waajiri walikua wanatulipa kwa hundi … utaratibu huu ulikua na changamoto nyingi,” amesema Badru katika mkutano huo uliokua na washiriki takribani 1,500.

“Kusema kweli, mwendo wetu ulikua kama wa kobe lakini hivi sasa uombaji na urejeshaji mikopo unafanyika kwa mtandao baada ya wataalamu wetu kutengeneza mifumo kwa kushirikiana na watalaam kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ambao tunawashukuru kwa ushirikiano,” amesema Badru.